CHAKULA CHA KUKU

Lishe bora kwa kuku ni jambo muhimu sana ili kuwezesha kuku wako kukua kwa haraka na pia kuepusha kuku kupatwa na magonjwa

Tunatoa ushauri wa namna ya kutengeneza chakula sahihi kinachofaa kwa ukuaji bora wa kuku

Tumia michanganuo hii kuchanganya chakula cha kuku wako

Mchanganyiko wa chakula cha vifaranga na kuku wadogo (Siku 1 mpaka wiki 8)

AINA YA VYAKULAKIASI (KILO)
Pumba za mtama, mahindi, uweleKilo 70
Mashudu ya, alizeti, , ufuta karanga au pamba n.kKilo 20
Unga wa mifupa au chokaa ya kukuKilo 3
Dagaa au mabaki ya samakiKilo 10
Chumvi ya jikoniNusu Kilo
Virutubisho (Premix)Robo Kilo
JUMLAKILO 103.75

Mchanganyiko wa chakula cha kuku wa miezi miwili na kuendelea

AINA YA VYAKULAKIASI (KILO)
Pumba za mtama, mahindi, uweleKilo 70
Mashudu ya, alizeti, , ufuta karanga au pamba n.kKilo 20
Unga wa mifupa au chokaa ya kukuKilo 3
Dagaa au mabaki ya samakiKilo 6
Chumvi ya jikoniNusu Kilo
Virutubisho (Premix)Nusu Kilo
JUMLAKILO 100